IQNA

21:35 - August 31, 2021
Habari ID: 3474243
TEHRAN (IQNA)- Mkutano wa 31 wa Mfumo wa Kiislamu wa Iran umeanza hapa Jumanne hapa Tehran.

Mkutano huo wa siku mbili unahudhuriwa na wakurugenzi wakuu wa benki zote nchi katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, maprofesa wa vyuo vikuu, na wachambuzi wa fedha, pamoja na maafisa wakuu wa serikali wakiwemo Gavana wa Benki Kuu ya Iran (CBI) Akbar Komeijani na Waziri wa Fedha na Uchumi Maswala Ehsan Khandouzi.

Katika mkutano huu, maswala kama vile usimamizi wa benki, marekebisho ya sheria za benki, mfumo wa biashara ya benki na jukumu la benki kusaidia uzalishaji wa ndani yanajadiliwa .

Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa mkutano huo, Gavana wa Benki Kuu ya Iran Komeijani alionyesha mwelekeo wa kuimarika thamani ya sarafu ya kitaifa dhidi ya dola ya Marekani, na akasema hali hii itaendelea katika miezi ijayo.

Pia alitaja kutengwa fedha za kigeni kwa ajili ya uagizaji wa chanjo za COVID-19, na kubainisha: "Mwaka jana, hatua zilichukuliwa kutenga fedha za kigeni zinazohitajika kutoa chanjo za COVID-19, na mchakato huu umeongeza kasi katika miezi ya hivi karibuni, na sasa hakuna shida katika suala hili. ”

Komeijani pia alisisitiza jukumu muhimu la mfumo wa kibenki katika kufadhili serikali na kutambua matarajio ya mapato ya muswada wa bajeti, na akasema: "Mwaka jana, Benki Kuu iliuza nyaraka za dhamana za Kiislamu zenye thamani ya karibu dola bilioni 30, ambazo asilimia 51 zilinunuliwa na benki na zilizosalia na watu binafsi soko la fedha; hii ilikuwa fursa  nzuri ya kumaliza nakisi ya bajeti. ”

Aidha amesema leo, teknolojia mpya zimewezesha mameneja na wasimamizi wote wa benki kufuatilia michakato mbalimbali ya benki na kuongeza kuwa, ‘teknolojia kama sarafu ya dijitali inaruhusu benki kuu kuzuia utoroshaji wa pesa na ukwepaji wa ushuru kwa kudhibiti mtiririko wa pesa nchini.’

/3475596

Kishikizo: benki za kiislamu ، iran
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: