IQNA

19:10 - May 06, 2022
Habari ID: 3475215
TEHRAN (IQNA)- Maimamu na wahubiri misikitini nchini Misri sasa watapata mafunzo maalumu kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii, intaneti na mabadiliko ya kidijitali.

Mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha kuimarisha uwezo wao na kutumia ipasavyo teknolojia za kisasa za habari na mawasiliano.

Mafunzo hayo ya ambayo pia yatajumuisha utumizi wa kompyuta yataanza Jumamosi katika Akademia ya Wakfu wa Kimataifa wa Kutoa Mafunzo kwa Maimamu mjini Giza.

Wizara ya Wakfu ya Misri imesema baada ya mafunzo hayo maimamu na wafanyakazi wa wizara hiyo watakuwa na uwezo wa hali ya juu wa kielimu katika ugawa wa teknolojia ya habari na mawasiliano.

Waziri wa Wakfu Misri Sheikh Mokhtar Gomaa alifungua Akademia ya Wakfu wa Kimataifa wa Kutoa Mafunzo kwa Maimamu (IAA) mwezi Januari.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa taasisi hiyo, alisema itakuwa na nafasi muhimu katika kutoa mafunzo ya Kiislamu yenye lengo la kukabiliana na wale wenye misimamo mikali na wanaopotesha mafundisho ya Kiislamu.

3478782

Kishikizo: misri ، misikiti ، dijitali ، intaneti
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: