IQNA

Harakati za mapambano Palestina zapongeza kutoroka jela mateka wa Palestina katika jela za Israel

19:05 - September 06, 2021
Habari ID: 3474266
TEHRAN (IQNA)- Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, amesema kuwa, hatua ya mateka 6 wa Kipalestina ya kutoka kwenye jela ya utawala wa Kizayuni licha ya kuweko ulinzi mkali, ni ya kishujaa.

Fawzi Barhoum amesema hayo na kuongeza kuwa, huo ni ushindi wa kweli na ni changamoto nzito kwa taasisi za usalama za utawala wa Kizayuni ambazo licha ya kuweka sheria kali, ulinzi mkubwa na ukatili wa kuchupa mipaka, lakini wameshindwa kuwazuia mashujaa hao wa Palestina kukimbia katika jela ya Wazayuni.

Amesema, kufanikiwa mateka hao wa Palestina kutoroka mikononi mwa makucha ya wanajeshi wa Israel kumethibitisha kwamba, adui Mzayuni kamwe hatoshinda licha ya kutumia nguvu za kila namna na ukatili usio na mfano. Mapambano ya wananchi wa Palestina yataendelea hadi watakapokomboa kila shibri ya ardhi yao inayokaliwa kwa mabavu na walowezi wa Kizayuni.

Kabla ya hapo pia, harakati ya Hamas pamoja na za Jihad al Islami na Mujahidina wa Palestina zilitoa taarofa tofauti na kuwapongeza mateka hao wa Kipalestina kwa kufanya ushujaa wa kutoroka kwenye jela ya Wazayuni. Harakati hizo tatu za mapambano za Palestina aidha zimesema kwenye taarifa zao kwamba huo ni ushindi mkubwa kwa taifa la Palestina kwani kuna ulinzi mkubwa na mkali sana katika jela za Wazayuni lakini pamoja na hayo, wanamapambano hao wa Palestina wamefanikiwa kutoroka.

Mateka 6 wa Palestina waliokuwa wanashikiliwa katika jela ya kutisha ya Gilboa ya Kizayuni iliyoko kaskazini mwa ardhi za Palestina zilizopachikwa jina bandia la Israel, wamefanikiwa kutoroka kwenye jela hiyo baada ya kuchimba makumi ya njia za chini ya ardhi.

Fawzi Barhoum : Kutoroka jela mateka wa Palestina ni hatua ya kishujaa

تمجید گروه‌های مقاومت از عملیات پیروزمندانه فرار 6 فلسطینی از زندان فوق امنیتی اسرائیل

تمجید گروه‌های مقاومت از عملیات پیروزمندانه فرار 6 فلسطینی از زندان فوق امنیتی اسرائیل + عکس

3995443

captcha