IQNA

Msomi wa DRC: Ukosefu wa umoja ni chanzo cha chuki dhidi ya Uislamu

18:00 - October 27, 2021
Habari ID: 3474478
TEHRAN (IQNA) – Mwakilishi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa (SAW) katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amesema maadamu hakuna umoja halisi katikaumma wa Kiislamu basi maadui watazidi kueneza chuki dhidi ya Uislamu duniani.

Katika mahojiano na IQNA pembizoni mwa Kongamano la 35 la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu ambalo lilifanyika wiki iliyopita, Sheikh Ismail Bukasa amesisitiza umuhimu wa umoja na mshikamano miongoni mwa Waislamu.

Aidha amesema Waislamu wanapaswa kushirikiana pamoja katika masuala mbali mbali na kwamba umoja na mifarakano uhudhuru Uislamu na Waislamu.

Bukasa ambaye pia ni mwanaharakati wa Haki za Binadamu amesema iwapo Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni watafanyakazi pamoja na kushirikiana katika ustawi na maendeleo huku kila moja akishikilia itikadi zake, ziwe ni za Kishia au Kisunni, basi hilo litakuwa bora kwa Waislamu, wote.

Halikadhalika amesema mifarakano baina ya Waislamu hupelekea maadui kutumia furs ahiyo kuibua  chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) na jambo hilo ni pigo kwa Waislamu. Amebaini kuwa kuna haja kwa Waislamu wote kushirikiana katika  kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu. Pia amepongeza jitihada za Kongamano la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu ambalo hufanyika kila mwaka na kusema kongamano hilo lina nafasi muhimu katika kuwaleta Waislamu pamoja.

Mkutano wa 35 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu ulifanyika kuanzia 19 hadi 23 mjini Tehran kwa kaulimbiu ya "Umoja wa Kiislamu; Amani na Kuepukana na Mifarakano na Mizozo" kwa hotuba ya Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Mkutano huo wa siku tano, ambao kwa sababu ya kuchunga miiko na miongozo ya kiafya ya kujiepusha na janga la corona unafanyika kwa mahudhurio ya moja kwa moja na kwa njia ya intaneti, unahudhuriwa na washiriki kutoka Iran na nchi 39 duniani.

4007271

captcha