IQNA

Juzuu ya 30 ya maandishi ya Braille yachapishwa Kuwait

23:55 - September 09, 2021
Habari ID: 3474279
TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Kuchapisha Qur’ani Tukufu nchini Kuwati imechapisha Juzuu ya 30 ya Qur’ani Tukufu kwa hati za Baraille au maandishi nukta nundu.

Maandishi ya nukta nundu hutumiwa na watu wenye ulemavu wa macho.

Mwanachama mwandamizi wa jumuiya hiyo, Mubarak al Hayan amesema Juzuu ya 30 ya Qur’ani Tukufu ambayo pia ni maarufu kama Juzu Amma, imechapishwa kwa maandishi ya nukta nundu kwa kushirikiana na Kituo cha Walemavu wa Macho Kuwait.

Amesema nakala hizo maalumu za Juzu Amma zitasambazwa kwa wale wenye ulemavu wa macho nchini humo na maeneo mengine duniani.

AL Hayan amesema  wanapanga kuchapisha vitabu vingine vya Kiislamu na Sunnah ya Mtume Muhammad SAW kwa kutumia  maandishi ya nukta nundu.

3995971

ما هو نظام برايل؟ - تفكر

 

captcha