IQNA

Wanawake kuruhusiwa tena kusali misikitini UAE

22:29 - November 10, 2021
Habari ID: 3474539
TEHRAN (IQNA)- Wakuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu wametangaza kuwa, wanawake sasa wataruhusiwa tena kusali misikitini baada ya maeneo yao kufungwa kwa muda kutokana na janga la COVID-19.

Pamoja na kuwa misikiti ilifunguliwa tena nchini UAE Disemba mwaka jaana baada ya kufungwa kwa muda mrefu kutokana na janga la COVID-19 maeneo ya wanawake misikitini yalikuwa yangali yamefungwa.

Sasa kumbi za wanawake kusali zimefunguliwa kama ambavyo pia maeneo ya kutawadha na vyoo navyo pia vimefunguliwa. Hatahivyo waumini wametakuwa kuzingatia maelezo ya kiafya yaliyowekwa ili kuzuia kuenea COVID-19.

Daktari Saif Al Dhaheri Msemaji wa Mamlaka ya Kitaifa ya Kukabiliana na Maafa amesema misikiti yote itafungwa punde baada ya kila sala.

/3476424

captcha