IQNA

Msikiti mkubwa zaidi Scotland kutumia nishati ya jua

17:21 - November 09, 2021
Habari ID: 3474535
TEHRAN (IQNA) - Msikiti Mkuu wa Glasgow, Scotland, ambao unatambuliwa kuwa moja ya misikiti ya kijani zaidi duniani kwa maana kuwa unazingatia utunzaji mazingira katika shughuli zake, sasa utaanza kutumia nishati ya jua kikamilifu.

Mradi huo wa nishati ya jua ambao umefadhiliwa na shirika la misaada la Islamic Relief ulitangazwa Alhamisi wakati wa kongamano la kimataifa la mabadiliko ya tabia nchi la COP26 ambalo linaendelea mjini Glasgow. Katika mradi huo mabati ya nishati ya jua yapatayo 130 yatawekwa katika msikiti huo na hivyo kuchangia katikak kupunnguza kilo 18,000 za hewa chafu aina ya CO2 kwa mwaka ittokanayo na utumizi wa nishati zingine.

Kutokana na jitihada hizo, msikiti huo wa Glasgow unatumiwa kama mfano wa kuigwa katika kuhimiza misikiti mingine duniani itumie nishati ya miale ya jua ili kutunza mazingira na kupunguza gharama.  Inatazamiwa kuwa mradi kama huo utatekelezwa katika  misikiti ya Masjid Al Haram mjini Makka, Masjid Al Nabawi mjini Medina, na Masjid  Al Azhar Mosque mjini Cairo.

Msimamizi wa mradi huo wa Msikiti Mkuu wa Glasgow anasema mradi huo unaonyesha kuwa umma wa Waislamu uko mstari wa mbele katika kulinda mazingira ya sayari ya dunia. Naye katibu mkuu wa msikiti huo Irfan Razzaq anasema ni jukumu la Waislamu kulinda mazingira kwa ajili ya vizazi vijavyo kwa kuacha kutumia nishati ambazo zinaharibu mazingira.  

4011500

 

Glasgow mosque goes green with solar energy panels

 

Al Fozan

4011500

Kishikizo: glasgow scotland msikiti
captcha