IQNA

Idhaa ya Qur'ani Tunisia, 'Radio Zaitouna' sasa inamilikiwa na serikali

16:49 - November 14, 2021
Habari ID: 3474558
Idhaa ya Qur'ani Tunisia, 'Radio Zaitouna' sasa inamilikiwa na serikali

Mhusika katika mchakato huo, Muhammad al Saidi, amesema tartibu zote za Radio Zaitouna kujiunga na Radio ya Kitaifa ya Tunisia zimekamilika baada ya mapatano kutiwa saini Ijumaa.

Hivi sasa Radio Zaitouna inakuwa stesheni ya 11 ya Televisehni ya Kitaifa ya Tunisia.  Kwa mujibu wa mapatano yaliyofikiwa Disemba 2020, Radio Zaitouna itaendelea kuwa huru katika kazi zake na haitahusishwa katika migogoro ya kisiasa au mashinikizo kutoka makundi mengine.

Radio Zaitouna ilianzishwa Septemba 2007 kama radio ya kwanza ya Kiislamu nchini Tunisia.

4013118

Kishikizo: tunisia ، radio ، zaitouna ، qurani
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha