IQNA

Kamanda Mkuu wa IRGC

Njama za adui katika Ulimwengu wa Kiislamu zimefeli kutokana na busara ya Kiongozi Muadhamu

20:45 - September 29, 2020
Habari ID: 3473214
TEHRAN (IQNA) - Meja Jenerali Hussein Salami, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesema kuwa, tadbiri na busara za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu zimefelisha njama na malengo ya kisiasa ya adui katika Ulimwengu wa Kiislamu.

Kamanda Salami ameashiria uadui dhidi ya taifa la Iran na vita vya kulazimishwa vya miaka minane vilivyoanzishwa na utawala wa dikteta Saddam dhidi ya Iran ya Kiislamu na kueleza kwamba, kutokuogopa kifo wananchi ndio siri ya kupata ushindi; kwani asiyeogopa vita katu hawezi kushindwa.

Meja Jenerali Salami ametanabahisha kwamba, vita vimemalizika lakini njama na vitendo vya kiuadui dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran havijamalizika. Amesema, busara na tadbiri za Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu zimefelisha njama za maadui na kuwafanya washindwe kufikkia malengo yao ya kisiasa katika Ulimwengu wa Kiislamu.

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) ameongeza kuwa, hii leo wigo wa kujihami kutakatifu umepanuka na vijana katika Ulimwengu wa Kiislamu  wamejifunza muqawama kupitia kujihami kutakatifu kwa Iran katika vita vya kulazimishwa vya miaka minane.

Meja Jenerali Salami ameashiria vikwazo vya kila upande dhidi ya Iran na kueleza kwamba, maadui wameanzisha vita vya kiuchumi na mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa, lakini kiongozi wetu, Ayatullah Khamenei amesimama kidete na anatambua siri ya kumshinda adui.

3926132

Kishikizo: iran ، IRAN irgc ، salami ، kiislamu
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :