IQNA

Mamia wahitimu kuhifadhi Qur'ani nchini Uturuki

11:44 - December 12, 2021
Habari ID: 3474668
TEHRAN (IQNA)- Mahafali ya kuhitimu mamia ya wanafunzi walioifadhi Qur'ani Tukufu imefanyika kaskazini mashariki mwa Uturuki katika mkoa wa Rize.

Jumla ya wanafunzi 571, wakiwemo 149 wa kike walipokea vyetu vya kuhitimu kuhifadhi Qur'ani Tukufu katika mahafali hiyo iliyofanyika Ijumaa.

Wanafunzi hao wamehifadhi Qur'ani kikamilifu na wamekuwa wakisoma chini ya usimamizi wa Taasisi ya Darul Iftaa mkoni humo.

Akihutubu katika sherehe hiyo, ambayo ilihudhuriwa na waalimu na wazazi, Naibu Mkuu wa Idara ya Masuala ya Kidini Uturuki amesema Qurani Tukufu inawaongeza wanaadamu katika amani na maadili mema.

Amesema wale wanaohifadhi Qur'ani wana nafasi muhimu katika kueneza lugha ya Kiarabu nchini humo huku akisisitiza umuhimu wa kutekeleza kivitendo mafundisho ya Qur'ani.

3476891

 
captcha