IQNA

Utawala wa Israel wamuachilia huru Sheikh Salah kiongozi wa Harakati ya Kiislamu

22:41 - December 13, 2021
Habari ID: 3474669
TEHRAN (IQNA)- Utawala wa Kizayuni wa Israel umemuachilia huru iongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Palestina Sheikh Raed Salah.

Imedokezwa kuwa, Sheikh Salah ameachiwa huru leo baada ya kuhudumi miezi 18 kati ya miezi 28 aliyohukumiwa gerezani.

Mwanazuoni huo maarufu wa Kiislamu na mtetezi wa haki za Palestina alikuwa anashikiliwa katika jela ya kuogofya ya utawala wa Kizayuni ya Megiddo. Mamia ya wakazi wa mji wa Umm al-Fahm wamemlaki kwa vifijo mkuu huyo wa Harakati ya Kiislamu katika ardhi za Palestina zilizoghusubiwa mwaka 1948 ambazo zimepachikwa jina bandia la Israel.. 

Sheikh Salah alitumia nusu ya kifungo chake cha miezi 28 katika seli ya mtu mmoja ya jela ya Israel.  

Utawala wa Kizayuni wa Israel mwezi Novemba mwaka 2015 uliitangaza Harakati ya Kiislamu inayoongozwa na Sheikh Raed Salah kuwa kundi la kigaidi linaloendesha harakati zake kinyume cha sheria kutokana na muqawama na mapambano ya harakati hiyo ya Kiislamu huko Quds inayokaliwa kwa mabavu na katika kutetea Msikiti wa al Aqsa. 

Wapalestina zaidi ya 4,650 wanashikiliwa katika jela za utawala wa Kizayuni, 180 miongoni mwao wakiwa ni watoto. 

4020593

captcha