IQNA

Ayatullah Sistani akutana na watoto wanaougua saratani

20:12 - December 15, 2021
Habari ID: 3474679
TEHRAN (IQNA)- Watoto kadhaa wanaougua saratani wamekutana na mwanazuoni wa ngazi za juu wa Mashia nchini Iraq Ayatullah Sayyid Ali al Sistani.

Watoto wamekutana na mwanazuoni huyo wakiwa wameandamana na madaktari na wauguzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Onkolojia ya Warith inayofungamana na Idara ya Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Hussein AS.

Katika hafla hiyo, Haidar Hamza al Abidi, mkurugenzi wa taasisi hiyo, amemfahamisha Ayatullah Sistani kuhusu huduma wanazotoa kwa wagonjwa wa saratani.

Ayatullah al Sistani ameipongeza taasisi hiyo kwa kutoa huduma za kiafya kwa Wairaqi wote bila kujali itikadi au kaumu huku akipongeza jitihada za madaktari na wauguzi wa taasisi hiyo.

Katika kikao hicho, Jannat Imad Abdul Wahhab, msichana anayeugua leukemia amemshukuru Ayatullah Sistani kwa kuwasaidia wagonjwa na pia amepongeza Idara ya Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Hussein AS kwa kutoa huduma bila malipo kwa wagonjwa wa saratani.

4020928

captcha