IQNA

Ayatullah Makarem Shirazi: Uislamu hauafiki kupinga chanjo

16:26 - December 27, 2021
Habari ID: 3474728
TEHRAN (IQNA)- Mwanazuoni mwandamizi wa Kiislamu nchini Iran Ayatullah Nasser Makarem Shirazi amesema Uislamu unalipa uzito mkubwa suala la afya ya mwanadamu.

Akizungumza baada ya kudungwa dozi ya tatu ya chanjo ya COVID-19 katika mji mtakatifu wa Qum, Ayatullah Makarem Shirazi amesema kulinda afya ni wajibu katika Uislamu.

Aidha amesema wale ambao wanapinga chanjo wanakiuka mantiki ya Kiislamu uku akitoa wito kwa wote kutekeleza maagizo ya madaktari na kudungwa chanjo ya COVID-19 ili waliende afya zao.

Hadi sasas Wairani 59,52 kati ya million 83 wamepokea dozi ya kwanza ya COVID-19 huku milioni 51.25 wakiwa wamepata dozi zote mbili na wengine milioni 5.92 tayari wameshapata dozi ya tatu.

Hadi sasa watu 131, 434 wamepoteza maisha kutokana na COVID-19 nchini Iran huku dunia nzima vifo vikwa ni zaidi ya milioni 5.3.

84592204

captcha