Nishar Ali, mweka hazina wa Msikiti wa Palmerston North, amesema wameamua kuinga mkono serikali ili ifikie lengo la chanjo kwa asilimia 90 ya watu wote nchini humo.
Amesema kuwepo zoezi hilo la chanjo ndani ya Msikiti kunawafanya Waislamu waafikie kuchanjwa huku walio na maswali wanauliza bila kuwa na wasiwasi hata kama hawaelewi Kiingereza.
Kuna Waislamu 1500 eneo la Manawatu, na miongoni mwao ni wakimbizi 300 waliofika eneo hilo hivi karibuni na hivyo hawafahamu Kiingereza. Aidha katika msikiti huo wanawake Waislamu wanapata fursa ya kuchanjwa na wauguzi wanawake katika chumba tafauti na hivyo nukta hiyo imechangia kuongeza idadi ya wanaochanjwa.