IQNA

Kuhifadhi Qur'ani ni sharti kwa wanachama wa Jumuiya ya Wasomaji Qur'ani Misri

12:02 - December 30, 2021
Habari ID: 3474742
TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Wasomaji Qur'ani Tukufu Misri imeitisha mkutano hivi karibuni ambapo imeamuliwa kuwa wananchama wote wapya wanapaswa kuwa wamehifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.

Hayo yamedokezwa na mkuu wa jumuiya  hiyo Sheikh Mohammad Hashad , ambaye amesema kwa mujibu wa uamuzi huo, yeyote ambaye anataka kujiunga na jumuiya hiyo anapaswa kuwa amehifadhi Qur'ani moyoni kikamilifu.

Amesema humuiya hiyo ina wanachama 9,000 na kwamba yeyote atakayekiuka kanuni atafikishwa katika kamati ya nidhamu.

Aidha ametoa wito kwa wasomaji Qur'ani kuhakikisha kuwa wanaposhiriki katika hafla ya mazishi hakuna msongamano wa watu.

4024516

 

captcha