IQNA

Waislamu, Wakristo Cameroon washiriki dua ya amani, mafanikio AFCON

14:13 - January 08, 2022
Habari ID: 3474781
TEHRAN (IQNA)- Viongozi wa Kiislamu na Kikristo nchini Cameroon wameshiriki katika dua ya pamoja kuomba amani na mafanikio ya mashindano ya soka ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Kwa mujibu wa taarifa katika hafla hiyo iliyofanyika Januari 6 mjini Yaounde na kuhudhuria na Waziri Mkuu wa Cameroon Joseph Dion Ngute, viongozi hao walimuomba Mwenyezi Mungu afanikishe mashindano hayo ya AFCON yanayofanyika Januari 9 hadi Februari 2 2022.

Kiongzoi wa Kiislamu Sheikh Souleymane Bouba hasa ameombia pia amani katika maeneo ya kaskazini magharibi na kusini magharibu mwa Cameroon ambayo yamekuwa yakikumbwa na uasi.

Kwa kuzingatia kuwa mashindano ya AFCON yanafanyika wakati wa janga la COVID-19 kumekuwa na wasi wasi  kuhusu mafanikio ya kombole hilo.

Kombe la mataifa ya Afrika, linalojulikana rasmi kama CAN, pia linafahamika kama AFCON, ndiyo tukio kuu la mashindano ya kandanda ya shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika CAF.

4026960

Kishikizo: cameroon waislamu
captcha