IQNA

Wawakilishi wa Tanzania, Kenya, Uganda waingia fainali za mashindano ya Qur'ani Iran

16:03 - February 01, 2022
Habari ID: 3474877
TEHRAN (IQNA)-Wasimamizi wa Mashindano ya 38 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran wametangaza majini ya waliofika katika fainali ya mashindano hayo itakayofanyika mwezi ujao ambapo miongoni mwa waliofuzu ni wawakilishi wa Kenya na Uganda.

Duru za mchujo za mashindano hayo zimefanyika kwa miezi kadhaa kwa njia ya intaneti kwa kushirikiwa washindani kutoka nchi zaidi ya 60 duniani.

Kwa mujibu wa taarifa waliofuzu kushiriki katika fainali ya kawaida  katika kategoria ya qiraa ya Qur'ani Tukufu ni Zakaria al-Zirak wa Morocco, Hadi Movahed Amin wa Iran, Owais Ahmadian wa Afghanistan, Mohammad Vejahat Reza wa Pakistan, Ilham Mahmoud al-Din wa Indonesia Bilal Abdullah Ali wa Yemen, Yas Fadhl Jassem na kutoka Tajikistan ni Samareddin Samadev.

Katika kategoria ya Tartil waliofika fainali ni Seyed Hojjat Tarahomi wa Iran, Mohammad Sadeq Sohrabyar wa Afghanistan, Hussein Ibrahim Imam Muhammad wa Egypt, Musa Safani wa Algeria, Mustafa Zahed wa Morocco, Hamza Muhammad Faraj Salawati wa Libya, Omar Abu Hafs wa Syria na Gholam Mustafa Ashrafi wa Australia.

Waliofika fainali katika kategoria ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu ni Haitham Safar Ahmad kutoka Kenya, Mohammad Reza Jahedinia wa Iran, Hamza Fahzi wa Marekani, Hessan Mahmoud Bakour wa Syria, Muhammad Rafa’a al-Bina wa Indonesia, Hassan Jibril Omar kutoka Niger, Aman Adil Ali wa Uganda na Adbul Khaliq kutoka Afghanistan.

Kwa upande wa wanawake waliofika katika  fainali ya Mashindano ya Kiamtaifa ya Qur'ani ya Iran mwaka huu ni Rafda Farinda wa Indonesia, Zahra Abdul Jabbar wa Iraq, Ashura Amani kutoka Tanzania, Tahereh Naebi Movahed kutoka Iran, Shafa’a Isfou Muhammad wa Niger, Maryam Mukhtar wa Nigeria, Zaynab bin Yusuf wa Algeria na Khadija Kubra wa Bangladesh.

Katika kitengo cha wavulana waliofuzu fainali za qiraa ya Qurani Tukufu ni wawakilishi wa Brunei, Bangladesh, Nigeria, Jamhuri ya Congo, Iran, na Ivory Coast huku waliofanikiwa kufika fainali ya kuhifadhi wakiwa ni wawakilishi wa Afghanistan, Iran, Lebanon, Iraq, Sweden na Ujerumani.

Kwa upande wa kitengo cha wasichana waliofika fainali ya kuhifadhi Qurani ni wawakilishi wa Iran, Indonesia, Tanzania na Uturuki Turkey na waliofika fainali ya qiraa kitengo hicho ni wawakilishi wa Sri Lanka, Lebanon, Indonesia na Iran.

Katika kategoria ya wenye ulemavu wa macho upande wa wanawake katika mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran kutakuwa na wawakilishi wa Iran, Iraq, Algeria, Lebanon na India na upande wa wanaume kutakuwa na wawakilishi wa Syria, Iraq, Iran, Algeria na Bangladesh.

Fainali ya mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani imepangwa kufanyika mwezi 27 Rajab kwa mnasaba wa  Eid al-Mab’ath, ambayo ni siku ya kubaathiwa Mtume Muhammad SAW.

Mashindano hayo ya Qur'ani ya Kimataifa huandaliwa kila mwaka na Shirika la Wakfu la Iran.

4032769  

 

captcha