IQNA

Pendekezo la kuundwa taasisi ya kimataifa ya mashindano ya Qur'ani

18:01 - January 10, 2022
Habari ID: 3474791
TEHRAN (IQNA)- Afisa mwandamizi wa Shirika la Wakfu la Iran amesema kuna haja ya kuundwa taasisi ya kimataifa ya nchi zinazoandaa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani.

Katika mahojiano na Shirika la Habari la Mehram Mahdi Ghareh Sheikhlu, mkuu wa masuala ya Qur'ani katika Shirika la Wakfu la Iran, ambalo huandaa mashindano ya Qur'ani Iran, amesema jumuiya kama hiyo itakuwa na makao makuu ya kuratibu mashindano.

Ameongeza kuwa Shirika la Wakfu la Iran linafanya mashauriano ya kimataifa kuhusu kuundwa taasisi kama hivyo na hivi karibuni matokeo ya mashauriano hayo yatatangazwa.

Amesema taasisi hiyo itakuwa na jukumu la kutoa miongozo na kubadilishana uzoefu wa mashindano ya Qur'ani.

Aidha amesema hatua za awali za kuundwa taasisi hiyo zitatangazwa katika Mashidano ya 38 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran Jamhuri ya Kiislamu mwaka huu.

Mchujo wa mashindano hayo umeanza Jumapili kwa njia ya intaneti kwa kushirikisha wawakilishiwa nchi 69.

5325206

captcha