IQNA

16:08 - February 07, 2022
Habari ID: 3474900
TEHRAN (IQNA)- Fainali ya Mashindano ya 38 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran itafanyika kwa njia ya intaneti kama ilivyokuwa katika duru za mchujo.

Fainali hiyo itafanyika kuanzia Februari 28 hadi Machi 5 ambapo washiriki kutoka maeneo mbali mbali ya dunia watawasiliana kwa njia ya video na jopo la majaji ambalo litakuwa sehemu moja mjini Tehran.

Mbali na mashindano ya kawaida pia kutakuwa na duru ya tano ya mashindano ya kimataifa ya walemavu wa macho, na mashindano ya saba ya kimataifa ya wanafunzi wa shule na halikadhalika mashindano ya kimataifa ya wanawake.

Uamuzi wa kufanya mashindano hayo kwa njia ya intaneti umechukuliwa kutokana na ongezeko la maambukizi ya COVID-19 duniani. Washindao watatangazwa tarehe 27 Rajab kwa mnasaba wa Eid al Mabaath, siku aliyobaathiwa Mtume Muhammad SAW.

4034395

Kishikizo: fainali ، mashindano ya qurani ، iran
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: