IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Kulinda na kuhifadhi miti ni kazi muhimu sana ambayo inapaswa kufanywa

17:48 - March 06, 2022
1
Habari ID: 3475016
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kulinda na kuhifadhi miti ni kazi muhimu sana ambayo inapaswa kufanywa

Ayatullah Ali Khamenei amesema hayo leo baada ya kupanda miche ya miti ya matunda kwa mnasaba wa maadhimisho ya Wiki ya Maliasili na Siku ya Kupanda Miti nchini Iran ambapo amesema  kupanda miti ni harakati ya kidini na kimapinduzi kikamilifu na kuongeza kuwa, kulinda na kuhifadhi miti ni kazi muhimu sana ambayo inapaswa kufanywa.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema pia kuwa, mmea hai unaleta utulivu katika roho na kulinda mwili wa mtu na ni chimbuko la riziki na atia ya Mwenyezi ya kila upande kwa ajili ya jamii ya mwanadamu.

Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa, ni kwa sababu hiyo ndio maana kuharibu misitu na mazingira kunahesabiwa kuwa ni uharibifu wa manufaa ya taifa. Kadhalika amesema, kuharibu misitu kwa ajili ya ujenzi ukiondoa pale inapolazimu na kuwa ni dharura hapana shaka kuwa ni kwa madhara ya taifa.

Halikadhalika Kiongozi Muadhamu amesisitiza juu ya udharura wa kustawishwa nishati safi. Amesisitiza kwamba, kustawishwa nishati safi kama nishati ya nyuklia ambayo matumizi yake yamekuwa yakiongezeka duniani na nchi za Asia Magharibi pia zinaelekea huko na vilevile nishati ya upepo na jua ni mambo ambayo yanapaswa kupewa uzito.

Kulinda hifadhi za wanyama ni jambo jingine ambalo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelitaja kuwa kupuuzwa kwake ni kwa madhara kwa maslahi ya taifa na kuongeza kuwa, katika Uislamu uwindaji unaruhusiwa pale tu panapokuweko haja na hitajio la chakula na kinyume na hivyo hairuhusiwi, na ni uhalifu na hata safari ya kwenda kuwinda inahesabiwa kuwa safari ya haramu. Amesisitiza kuwa, ni kwa msingi huo ndio maana kuna haja ya kuchukuliwa hatua za maana kuzuia uwindaji haramu na kuzingatiwa suala la kulinda hifadhi za wanyama.

4040692

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
el maghriby
0
0
Hongera kiongozi wa Irani kwa kuonyesha mfano mwema wa kuhimiza Waislamu wapande miti. Ni hatua muhimu iliyosahauliwa na viongozi wengi wa kidini.
captcha