IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Upandaji miti ni alama ya heshima, mazingira yahifadhiwe

10:31 - March 09, 2017
Habari ID: 3470885
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Jumatano asubuhi amepanda miche miwili ya miti ya matunda katika maadhimisho ya Wiki ya Rasilimali za Maliasili nchini Iran.

Katika nasaha alizotoa mara baada ya shughuli hiyo ya upandaji miti, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameashiria umuhimu wa mandhari ya kijani kibichi na upandaji mimea na majani na kueleza kwamba taathira nyingi mbaya zinazotokana na tufani ya vumbi, uchafuzi wa hali ya hewa na kuwepo hewa chafu katika miji zinasababishwa na uhaba wa maeneo yenye mimea; na kwa kuzingatia hali ya kijiografia na kuongezeka maeneo yenye ardhi ya jangwa nchini suala la kutunza na kuendeleza upandaji mimea linakuwa na umuhimu maradufu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwepo maeneo ya kijanikibichi yenye anuai za mimea ya dawa za mitishamba pamoja na misitu ya eneo la Kaskazini mwa nchi ni miongoni mwa sifa kuu za mandhari za kijani za nchini Iran na akaongezea kwa kusema: Misitu yenye thamani ya Kaskazini ni miongoni mwa misitu ya nadra kushuhudiwa duniani, lakini baadhi ya watu wanaojali faida ya biashara tu hawatilii maananimaslahi ya taifa bali wanavamia misitu na rasilimali za nchi; hivyo lazima misitu hiyo ilindwe na uvamizi huo.

Ayatullah Khamenei aidha amesisitiza kuwa upandaji miti ni alama ya heshima ambayo wananchi wanayapa maeneo ya kijanikibichi ya ardhi ya Iran.

Tarehe 5 Machi kila mwaka huadhimishwa hapa nchini Iran kuwa ni Siku ya Upandaji Miti.

3582035

captcha