IQNA

Dhifa ya futari ya umma mjini Cape Town Afrika Kusini

12:51 - April 12, 2022
Habari ID: 3475117
TEHRAN (IQNA)- Wakaazi wa eneo moja Cape Town, Afrika Kusini, wamepewa zawadi dhifa ya futari kwa mara ya kwanza huku Waislamu duniani kote wakiwa katika mwezi mtakatifu wa Ramadan.

Wakati mtu anaposikia jina la mtaa wa Cafda katika eneo la Retreat mjini Cape Town, mara nyingi huhusishwa na unyanyasaji na uhalifu wa magenge. Hata hivyo, siku ya Jumapili wakati wa eneo hilo waliketi bega kwa bega wakati wa Iftar, kwa hisani ya msikiti na Waislamu wafadhili katika eneo hilo.

Iftar au futari ni chakula kinacholiwa na Waislamu baada kufunga kula na kunywa katika siku za mchana za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Hii ni mara ya kwanza kwa dhifa ya umma ya futari kuandaliwa katika eneo hilo.

Barabara ya Peter Charles ilifungwa kwa muda ili kuwawezesha watu zaidi ya 1 200, Waislamu na wasio Waislamu, kukusanyika ili kula pamoja.

Dhifa hiyo ya futari iliandaliwa na Msiki wa Masjid-Tul-Islamieya na taasisi za Carers Unite, Upcountry Feeding Hands, Shumeez Scott Foundation na Girls Feeding Scheme.

Dhifa za umma za futari ni mashuhuri pia katika mtaa wa Cape Flats  mjini Cape Town wakati wa Ramadhani ambapo barabara zimefungwa na watu kutoka kila tabakaa, dini na jamii wanaalikwa kujumuika kula na kuzungumza na wenzao katika jamii.

3478455

captcha