Wanafunzi wa kimataifa wa chuo hicho watawasilisha vyakula vya iftar kutoka nchi zao katika tamasha hili.
Wanafunzi hao wanawakilisha zaidi nchi 50 kutoka maeneo yote ya dunia
Naibu Waziri wa Sayansi, Utafiti, na Teknolojia wa Iran Saeed Habiba pamoja na baadhi ya watu mashuhuri na mabalozi kutoka nchi za Kiislamu nchini Iran watakuwepo katika tamasha hilo, ambalo limepangwa kufanyika Jumapili, Machi 9, 2025.
Iftar ni mlo wa jioni unaoashiria kumalizika saumu yaWaislamu katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani wakati wa adhana ya sala ya Maghribi.
Ramadhani ni mwezi wa tisa katika kalenda ya Kiislamu. Ni kipindi cha sala, kufunga, kutoa sadaka na kujihesabu kwa Waislamu kote ulimwenguni.
Wakati wa Ramadhani, Waislamu hufunga (kujizuia na chakula na vinywaji) kuanzia alfajiri hadi machweo wanapovunja mfungo wao.
/3492114