IQNA

Idadi ya wanaotaka kwenda Umrah mwezi wa Ramadhani yazidi kuongezeka

11:44 - March 10, 2022
Habari ID: 3475028
TEHRAN (IQNA)- Idadi ya Waislamu wanaokusudia kutekeleza ibada ya Hija ndogo au Umrah katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani inazidi kuongezeka.

Kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la Okaz la Saudi Arabia, maeombi ya kutoaka kutekekeza Ibada ya Umrah katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani imeongeza kwa kiwngo kikubwa.

Taarifa zinaonyesha kuwa waliowasilisha maombi ya Umrah kupitia aplikeshni za Eatmarna imeongezeka katika katika siku za Ijumaa za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani huku siku ya 30 ya mwezi huo ikiwa imejaa.

Mapema wiki hii Saudia ilitangaza kuondoa asilimia kubwa ya vizingiti vya corona ambapo hakuna tena sheria ya kutokaribiana kwa wanaosali katika Msikiti Mtakatifu wa Makka, Al Masjid Al Haramm  na Msikiti Mtakatifu wa Mtume SAW Masjid an-Nabawi,  mjini Madina.

Aidha gazeti hilo limeandika kuwa Saudia imefuta sharti la kipimo cha corona cha PCR kwa wale wanaowasili nchini humo. Aidha Saudia imeondoa marufuku ya wasafiri kutoka  Afrika Kusini, Namibia, Botswana, Zimbabwe, Lesotho, Eswatini, Msumbiji, Malawi, Mauritius, Zambia, Madagascar, Angola, Seychelles, Comoros, Nigeria, Ethiopia, na Afghanistan.

Mwezi Oktoba mwaka jana Saudia ilitangaza kuanza tena safari za Umrah baada ya kusitishwa kikamilfu kwa muda wa miezi saba kutokanga na janga la corona.

3478101

Kishikizo: umrah saudia
captcha