IQNA

Mijumuiko Mikubwa ya Futari yaruhusiwa tena Msikiti Mtakatifu wa Makka

19:16 - March 15, 2022
Habari ID: 3475045
TEHRAN (IQNA)- Mijumuiko mkiubwa ya futari itaruhusiwa tena katika Msikiti Mtakatifu wa Makka, Al Masjid Al Haram katika mwezi mtukufu wa Ramadhani baada ya kuzuiwa kwa muda wa miaka miwili kutokana na janga la COVID-19.

Idara ya Usimamizi wa Misikiti Miwili Mitakatifu imetangaza kuwa mipango ya ibada katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo sasa waumini wataruhusiwa kufuturi wakiwa ndani ya Masjid al Haram.

Mapema idara hiyo ilikuwa imetangaza kuwa mijumuiko ya futari imeruhiswa pia katika Msikiti Mtakatifu wa Mtume SAW, Masjid an-Nabawi,  mjini Madina.

Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unatazamiwa kuanza baada ya wiki mbili hivi na wakuu wa Saudi Arabia wameondoa aghalabu ya vizingiti vilivyokuwa vimewekwa katika maeneo ya ibada ili kuzuia kuenea COVID-19 au corona.

Haya yanakuja siku chache baada ya  uamuzi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudi kuondoa kanuni zilizokuwa zinatakelezwa za kuzuia kuenea corona zikiwemo za kutokaribiana waumini  Msikiti Mkuu wa Makkah, Msikiti wa Mtume SAW mjini Madina na misikiti mingine. Aidha si sharti tena waumini kuvaa barakoa.

Aidha si sharti tena kwa waumini wanaoenda Saudia kwa ajili ya Hija Ndogo au Umrah kuwa na chanjo ya corona au vipimo vya corona.

/3478181

captcha