IQNA

Ramadhani Marekani

New York: Sala usiku wa kwanza wa Mwezi wa Ramadhani katika Times Square

19:47 - March 11, 2024
Habari ID: 3478489
IQNA – Mwezi mtukufu wa Ramadhani ulipoanza, mkusanyiko mzuri wa waumini wa Kiislamu ulibadilisha Times Square ya New York kuwa eneo la umoja na ibada.

Makumi ya Waislamu walikusanyika Jumapili usiku kwa ajili ya Sala ya Taraweeh, ambayo husaliwa zaidi na Waislamu wa madhehebu ya Sunni kama sehemu muhimu ya ibada za usiku za katika Mwezi wa Ramadhani.

Salman al-Hanafy, mwendeshaji winchi mwenye umri wa miaka 20 kutoka Cairo, anabainisha hisia zake katika mahojiano na AFP: “Ni vizuri kuja hapa kama Waislamu. Niliona Waislamu kutoka kila mahali -- nilishangaa, ni mara yangu ya kwanza hapa. Nilitaka kuja kuona Waislamu wenzani.”

Hafla hiyo pia ilitumika kama daraja la kitamaduni, huku watu wa kujitolea wakisambaza nakala za Qur'ani Tukufu kwa Waislamu na wasio Waislamu vile vile.

Ahmad Yasar, mwanafunzi wa TEHAMA mwenye umri wa miaka 20, alikuwa miongoni mwa waliokuwa wakisambaza nakala za Qur'ani: "Watu wengi wanavutiwa na Qur'ani, karibu tumeishiwa na tafsiri za lugha ya Kifaransa. i,” alisema.

Licha ya baridi na upepo, waumini hawakukata tamaa, maombi yao yakiambatana na nyimbo za Nasheed na watoto wakisoma aya za Quran.

Mjumuiko  huo haukuwa tu tukio la kiroho bali pia maandamano ya mshikamano, huku bendera za Palestina zikipeperushwa kuonyesha uungaji mkono kwa Wapalestina Ukanda wa Gaza ambao wanakabiliwa na vita vya mauaji ya kimbari vya utawala haramu wa Israel.

Waandaaji walipata njia bunifu za kuboresha uzoefu wa ibada kwa kuandika aya na dua katika maeneo kadhaa jiji la New York.

3487516

captcha