IQNA

Mahema ya Futari kuweka tena UAE baada ya kupungua corona

20:42 - March 15, 2022
Habari ID: 3475047
TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) imetangaza kuidhinisha tena hema za futari wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani baada ya hema hizo kufungwa kwa muda wa miaka miwili kutokana na janga la corona au COVID-19.

Siku ya Jumatatu, Idara ya Kitaifa ya Kukabiliana na Majanga UAE imesema hema hizo sasa zinapaswa kurejeshwa. Taarifa ya idara hiyo imesema uamuzi huo umechukuliwa kama sehemu ya stratijia ya kitaifa ya kudumisha afya ya umma na kurejesha hali ya kawaida katika maisha.

Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu wa 1443 Hijria Qamaria unatazamiwa kuanza Aprili 2 2022 Miladia lakini  kuanza huko kutategemea taarifa za mwezi mwandamo nchini UAE na maeneo mengine duniani.

Kabla ya janga la corona, hema hizo ambazo kwa kawaida huwa pembizoni mwa msikiti hutumika kuwalisha vibarua wenye kipato cha chini.

3478182

Kishikizo: futari uae ramadhani
captcha