IQNA

Misri yatangaza zawadi wakatazopata washindi wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani

15:05 - June 05, 2022
Habari ID: 3475337
TEHRAN (IQNA) - Wizara ya Awqaf ya Misri imetangaza tuzo na masharti kwa washiriki wa Duru ya 29 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya nchi hiyo.

Katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumamosi, Waziri wa Wakfu Sheikh Mohammad Mokhtar Goma alitoa maelezo kuhusu masharti ya mashindano yajayo yatakayoanza Februari 4, 2023.

Amesema kwa msisitizo wa Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi, zawadi za juu katika baadhi ya kategoria zimeongezeka na kufikia Pauni 250,000 za Misri. Thamani ya chini ya tuzo ya juu ni Pauni 100,000 za Misri, alisema.

Waziri huyo alitaja alitaja kategoria nane za mashindayo hayo ambazo  zote zinalenga katika kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu, tafsiri na ufahamu wa Qur'ani.

Kategoria ya kwanza ni kuhifadhi Qur'ani na ufahamu wa aya zake kwa wanaume na wanawake walio chini ya umri wa miaka 45.  Mshindi wa kwanza na mshindi wa pili watapata Pauni 250,000 na 150,000 za Misri mtawalia.

Kundi la pili ni kuhifadhi Qur'ani na ufahamu wa aya zake kwa wanaoshiriki kama familia. Angalau watu watatu wa kila familia wanapaswa kuwa wamehifadhi Qur'ani Tukufu.  Familia bora itatunukiwa Pauni 250,000 za Misri.

Kategoria ya tatu  ni kuhifadhi, kufasiri na matumizi ya Qur'ani katika sayansi nyinginezo kwa washiriki walio chini ya umri wa miaka 45. Pauni 150,000 za Misri zitatolewa kwa mshindi.

Kategoria ya nna ni kuhifadhi Qur'ani Tukufu na kuweza kuisoma kwa mbnu zoe saba za qiraa kwa washiriki walio chini ya umri wa miaka 50 na zawadi ya juu itakuwa Pauni 150,000 za Misri.

Kundi la tano ni la kuhifdhi Qur'ani Tukufu  kwa wasiozungumza Kiarabu walio chini ya umri wa miaka 40 na zawadi ya juu ya Pauni 150,000 za Misri. Hafidh aliyeshika nafasi ya pili atapata Pauni 100,000 za Misri.

Kundi linalofuata ni kuhifadhi Qur'ani kwa watu wenye ulemavu. Washiriki wanapaswa kuwa na umri wa chini ya miaka 35 na mshindi wa kwanza atapata kitita cha Pauni 100,000 za Misri.

Kundi la saba ni la kuhifadhi Qur'ani na kuelewa msamiati na tafsiri yake kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 15. Pauni 100,000 za Misri zitatolewa kwa mshindi.

Kategoria ya mwisho ni ya washindi wote katika kuhifadhi Qur'ani Tukufu

Waziri huyo alifafanua kuwa matawi yote ya mashindano yapo wazi kwa wanaume na wanawake, ilimradi mshiriki hajawahi kushika nafasi ya kwanza au ya pili katika tawi lolote la shindano katika mwaka wowote uliopita.

3479173

captcha