IQNA

Ramadhani

Washindi wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Misri watunukiwa

11:58 - April 07, 2024
Habari ID: 3478644
IQNA - Washindi wa Awamu ya 30 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Misri wametunukiwa zawadi katika hafla ya Jumamosi.

Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi amewatunuku washindi katika hafla hiyo iliyofanyika na Wizara ya Wakfu katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Al Manara katika jiji jipya linalojulikana kama New Cairo.

El Sisi aliwatunuku washindi katika kitengo cha kwanza cha mashindano hayo, ambalo linajumuisha kuhifadhi Qur'ani nzima pamoja na usomaji wa Tajweed na kuelewa maana yake. Mshindi wa kwanza kutoka Gavana wa Beheira alijishindia zawadi ya EGP milioni moja.

Awamu ya 30 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani lilifanyika katika makundi sita, ikiwa ni pamoja na kuhifadhi Qur'ani nzima pamoja na qiraa na Tafseer (tafsiri), kuhifadhi Qur'ani kwa wasiozungumza Kiarabu, na kuhifadhi Qur'ani kwa maimamu wa sala na wahubiri.

Pia kulikuwa na kategoria ya kuhifadhi Qur'ani pamoja na ufahamu wa dhana zake kwa familia. Wawakilishi wa nchi 64 walishindana katika toleo la 30 la shindano hilo la kimataifa. Kulingana na Waziri wa Wakfu Mohamed Mukhtar Gomaa, jumla ya kiasi cha zawadi za fedha taslimu kwa toleo hili kilikuwa zaidi ya pauni milioni 8 za Misri, ikionyesha ukuaji wa asilimia 300 ikilinganishwa na toleo la mwaka jana.

3487837

captcha