IQNA

Jinai za Israel

Utawala wa Israel umeua waandishi habari 48 Gaza

22:04 - November 08, 2023
Habari ID: 3477860
TEHRAN (IQNA) - Mwandishi mwingine wa habari wa Kipalestina ameuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel huko Gaza huku vita vya utawala haramu wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza vikiendelea kwa muda wa zaidi ya mwezi mmoja.

Duru za Palestina zilisema Jumanne kwamba Yehya Abu Manie aliuawa katika shambulio la bomu la Israel katika mji wa Gaza, na kufikisha idadi ya waandishi wa habari 48 waliouawa tangu kuanza kwa vita vya maangamizi ya kimbari vya Israel dhidi ya Wapalestina tarehe 7 Oktoba.

Aidha utawala dhalimu wa Israel katika hujuma yake Gaza umelenga kwa mabomu zaidi ya majengo 50 ya vyombo vya habari na kuyaharibi kabisa au kiasi.

Maelfu ya watu waliingia katika mitaa ya Karachi, mji wa bandari wa kusini mwa Pakistan, Jumatano wakilalamikia "ukimya" wa nchi za Magharibi kuhusu mauaji ya raia, haswa watoto na waandishi wa habari, katika shambulio la anga la Israel kwenye Ukanda wa Gaza.

Mamia ya waandishi wa habari na familia zao walikusanyika katika Klabu ya Waandishi wa Habari ya Karachi ili kueleza mshikamano wao na wenzao wa Gaza waliouawa wakiwa kazini katika mashambulizi ya anga ya Israel huko Gaza tangu Oktoba 7.

Waandamanaji walikuwa wamebeba mabango yaliyoandikwa kauli mbiu kama vile "Acha kuwalenga waandishi wa habari," "Huwezi kuficha ukweli kwa kuwaua waandishi wa habari," na "Wajibisheni Israel kwa mauaji ya waandishi wa habari huko Gaza." 

Hayo yanajiri wakati ambao, Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa idadi ya waliouawa shahidi kutokana na mashambulio ya kinyama ya utawala wa Kizayuni katika eneo hilo imeongezeka na kufikia 10,569.

Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza leo (Jumatano, tarehe 8 Novemba) ikiwa ni siku ya 33 ya operesheni ya "Kimbunga cha Al-Aqsa" takwimu za karibuni kabisa za wahanga wa mashambulizi mtawalia ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa ripoti hii, idadi ya mashahidi wa vita vya Gaza katika siku ya 33 ya mashambulizi ya utawala huo ghasibu imefikia watu 10,569, kati yao 4,324 ni watoto na 2,823 ni wanawake.

Ashraf al-Qadra, msemaji wa Wizara ya Afya ya Palestina huko Gaza, ametangaza kwamba kesi  2550 zimesajiliwa  huko Gaza hadi sasa za watu waliopotea, ambapo 1,350 ni watoto na bado wako chini ya vifusi.

Habari zinazohusiana
captcha