IQNA

Waislamu Russia

Vyumba vya Waislamu kusali kujengwa katika barabara kuu za Russia

23:03 - June 16, 2022
Habari ID: 3475383
TEHRAN (IQNA)- Ofisi ya Mufti wa Jamhuri ya Tatarstan katika Shirikisho la Russia, kwa kushirikiana na Msikiti wa Ikhlas pamoja na moja ya mashirika ya vituo vya mafuta, imezindua mpango wa kujenga vyumba vya Waislamu kusali katika barabara kuu nchini humo.

Mradi huo ambao umepewa jina la ‘Sala ya Msafiri’  unalenga kuhakikisha kuwa Waislamu wana eneo bora la kusali wakiwa safarini bila tatizo lolote. Wiki iliyopita, chumba cha kwanza za Waislamu kusali kilifunguliwa katika Barabara ya M-17 katika kijiji cha Sine-Kinchery katika Jamhuri ya Chuvash.

Chumba hicho chenye ukubwa wa mita mraba 15 kina suhula zote ambazo Muislamu anahitaji wakati wa Sala ambapo watu 10 wanaweza kusali hapo wakati moja.

Wasimamizi wa mradi huo wanasema  kwa kuanzia wanalenga kujenga vyumba 24 vya Waislamu kusali katika barabara kuu za M-7 na M-5 katika maeneo saba ya Russia ambayo ni Vladimir, Penza and Nizhny Novgorod regions, Chuvashia, Mari El, Tatarstan na Bashkiria.

Russia ni nchi kubwa zaidi duniani yenye idadi ya watu milioni 146. Uislamu ni dini ya wachache nchini Russia ambapo kuna takriban Waislamu milioni 25. Nchi hiyo ina Waislamu wengi zaidi barani Ulaya. Raia wengi wa Russia ni Wakristo wa dhehebu la Orthodox. Kutokana na idadi kubwa ya Waislamu Russia, nchi hiyo ni mwanachama mwangalizi katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu (OIC).

4064743

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha