IQNA

Jinai za Israel

Indhari ya EU kuhusu Israel kuwafukuza Wapalestina Masafer Yatta

15:44 - July 08, 2022
Habari ID: 3475476
TEHRAN (IQNA) - Mwanadiplomasia mwandamizi wa Umoja wa Ulaya ameelezea wasiwasi wake kuhusu uwezekano idadi kubwa ya Wapalestina kuhamishwa kwa nguvu kutoka eneo la mashambani katika Ukingo wa Magharibi linalokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Sven Kuehn von Burgsdorff, balozi wa Umoja wa Ulaya huko Palestina, ameonya kwamba hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel kuwahamishwa kwa nguvu Wapalestina itakuwa ni "uhamisho mkubwa zaidi wa nguvu kwa miongo kadhaa."

Sven Kuehn von Burgsdorff, ametoa tahadhari hiyo baada ya kuzurua eneo Masafer Yatta kusini mwa Ukingo wa Magharibi, ambapo kufukuzwa kwa Wapalestina kumeongezeka baada ya uamuzi wenye utata wa mahakama ya utawala haramu Israel mwezi Mei.

Mahakama kuu ya utawala wa Tel Aviv ilitoa uamuzi tarehe 4 Mei kwamba zaidi ya wakazi 1,000 wa vijiji vya Masafer Yatta "wameshindwa kuthibitisha" madai yao ya makazi ya kudumu katika eneo hilo kabla ya jeshi la Israel kulitangaza kuwa ni eneo maalumu la mazoezi ya kijeshi, ambapo uwepo wa raia ni marufuku.

Von Burgsdorff alisisitiza kwamba kumekuwa na ongezeko kubwa la ubomoaji tangu uamuzi huo, huku chanzo cha Umoja wa Ulaya kikisema kuwa majengo 27 yamebomolewa na angalau maagizo 30 zaidi ya kubomoa yametolewa -- zaidi ya mara mbili ya kiwango katika miaka ya hivi karibuni.

Mwanzoni mwa miaka ya 1980, jeshi la Israel lilitangaza eneo hilo la kilomita 30 za mraba kuwa eneo la kijeshi lililowekewa vikwazo na kudai kuwa halikaliwi na watu huku Wapalestina waliokuwa wakiishi humo wakisema ni makazi ya watu wao muda mrefu kabla ya vikosi vya Israel vinavyokalia kwa mabavu kukanyaga Ukingo wa Magharibi.

Von Burgsdorff amesema majaji wakuu wa Israel wamepuuza sheria za kimataifa katika hukumu hiyo ambayo "inaonekana kupuuza" majukumu ya utawala huo kwa wakaazi wa Palestina kama "nguvu inayokalia kwa mabavu."

Tayari Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imetangaza kuwa kufukuzwa kwa Wapalestina kutoka eneo la Masafer Yatta, kusini mwa Ukingo wa Magharibi, kunaweza kuwa sawa na kuwalazimika kuyahama makazi yao, jambo ambalo ni ukiukaji mkubwa wa Mkataba wa Nne wa Geneva na hivyo kuzingatiwa kuwa ni uhalifu wa kivita.

Zaidi ya Waisraeli 600,000 wanaishi katika vitongoji zaidi ya 230 vilivyojengwa tangu mwaka 1967 Israel iliyakalia kwa mabavu maeneo ya Wapalestina ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na al-Quds Mashariki. Makaazi yote ya Waisraeli ni kinyume cha sheria za kimataifa kwani yamejengwa kwenye ardhi inayokaliwa kwa mabavu. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani shughuli za Israel za kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu.

3479616

captcha