IQNA

Jinai za Israel

Hamas yailaani Israel kwa kujenga vitongoji zaidi vya walowezi wa Kizayuni Quds

21:18 - August 18, 2022
Habari ID: 3475640
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imelaani vikali kuendelea kupasishwa mipango ya ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kkwa mabavu za Palestina.

Taarifa ya Hamas imesisitiza kuwa, ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Palestina ni juhudi za Israel baada ya kushindwa njama zake za kufuta alama za Kiislamu huko Quds.

Sehemu nyingine ya taarifa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imeeleza kuwa, wananchi wa Palestina chhini ya kivuli cha umoja watatumia kila nguvu na mbinu kwa ajili ya kukabiliana na jinai za adui Mzayuni.

Hamas imewataka wananchi wa Palestina kushikamana na subira na kuhakikisha kuwa, wanaendeleza mapambano yao dhidi ya utawala ghasibu wa Israel unaotenda jinai kila uchao dhidi ya wananchi wa Palestina.

Utawala huo ulizikaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina katika vita vya mwaka 1967;  na azimio la Geneva linasema kuwa ni marufuku utawala wa Kizayuni kufanya shughuli zozote za ujenzi katika ardhi hizo zinazokaliwa kwa mabavu. 

Hayo yanaripotiwa katika hali ambayo, hadi sasa utawala wa Israel haujachukua hatua yoyote ya kutekeleza azimio nambari 2234 la tarehe 23 Disemba 2016 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka kusitishwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu. 

4078963

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha