IQNA

Msikiti wa Al Aqsa

Siku ya Kimataifa ya Msikiti yaadhimishwa

14:31 - August 21, 2022
Habari ID: 3475658
TEHRAN (IQNA)- Leo 21 Agosti inatambuliwa kama Siku ya Kimataifa ya Msikiti kwa mnasaba wa kukumbuka tukio chungu la Agosti 21, 1969 wakati Mzayuni Michael Dennis Rohan alipoitekteza moto sehemu ya Msikiti wa Al Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu.

Utawala wa Kizayuni wa Israel ulidai kuwa, kitendo hicho kilifanywa na mtalii wa Kiaustralia. Utawala huo wa Kizayuni ulitayarisha mahakama ya kimaonyesho tu mjini Tel Aviv na kuchukua uamuzi wa kumuachilia huru mhalifu huyo kwa madai kwamba alikuwa na matatizo ya kiakili. Baada ya kutokea kitendo hicho, nchi za Kiislamu zilikutana na kuamua kuunda Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC).

Upasishwaji wa Siku ya Kimataifa ya Msikiti ulijiri mwaka 1382 Hijiria Shamsia, sawa na tarehe 22 Agosti mwaka 2003 Miladia katika mkutano uliofanyika mjini Tehran na kwa pendekezo la Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu la nchini Iran (ICRO) sanjari na kupitishwa na Wizara za Mashauri ya Kigeni za nchi za Kiislamu. Kikao hicho kilifanyika kwa mnasaba wa wiki ya kumbukumbu ya kuchomwa moto msikiti wa Al-Aqsa na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel tarehe 21 Agosti mwaka 1969 katika mji wa Quds (Jerusalem). Aidha katika kikao hicho nchi za Kiislamu zilitakiwa kutoa himaya kwa misikiti kama mahala patakatifu sanjari na kuienzi sehemu hiyo.

Quds na maeneo yake matakatifu yamekuwa yakishambuliwa na kuvunjiwa heshima tangu Wazayuni walipovamia na kukalia kwa mabavu ardhi ya Palestina. Katika kipindi chote cha miongo kadhaa iliyopita utawala wa kikatili wa Israel si tu kwamba hauwaonei huruma watoto wadogo na wanawake na umekuwa ukifanya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, bali pia umekuwa ukivunja na kuhujumu misikiti na makanisa ya eneo hilo. Pamoja na hayo Msikiti wa al Aqsa ndio unaoshambuliwa na kuvunjiwa heshima zaidi kati ya maeneo yote matakatifu ya Palestina na hilo linafanyika ili kuuharibu kabisa msikiti huo na hatimaye kufuta kabisa utambulisho wa kihistoria wa Palestina. Utawala bandia wa Israel daima umekuwa ukilipa kipaumbele suala la kufuta utambulisho wa Kiislamu wa Quds tukufu na kuharibu maeneo matakatifu na ya kihistoria ya mji huo.

4079597

captcha