IQNA

Jinai za Israel

HAMAS: Udhaifu wa nchi za Kiarabu unapelekea Israel kudhibiti Msikiti wa Al Aqsa

14:27 - September 27, 2022
Habari ID: 3475846
TEHRAN (IQNA)- Mjumbe mwandamizi wa ofiisi ya kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, utawala haramu wa Israel unatumia vibaya udhaifu ambao umeugubika ulimwengu wa Kiarabu na hivyo kuudhibiti mji wa Quds (Jerusalem) na msikiti mtakatifu wa al-Aqsa ulio mjini humo.

Mahmoud al-Zahar ameeleza kuwa, hujuma na uvamizi wa wanajeshi na walowezi wa Kiyahudi dhidi ya msikiti wa al-Aqsa ni sera zinazotekelezwa na wavamizi katika kivuli cha himaya ya Mayahudi katika ulimwengu wa Magharibi na kutumia vibaya udhaifu wa kusikitishwa wa madola ya Kiarabu.

Kiongozi huyo wa ngazi za juu wa chama cha Hamas amesisitiza kuwa, njia pekee ya kukabiliana na hujuma na jinai za utawala dhalimu wa Israel ni muqawama na mapambano.

Tangu jana Jumatatu walowezi wa Kiyahudi wameshadidisha hujuma na uvamizi wao dhidi ya msikiti wa al-Aqswa kwa kisingizio cha kuanza mwaka mpya wa Kiyahudi.

Wanajeshi wa Israel wamekuwa wakitoa himaya na kusaidia walowezi hao katika hujuma zao sambamba na kukabiliana na vijana wa Kipalestina wanaojitokeza kuuhami na kuulinda msikiti huo mtakatifu kibla cha kwanza cha Waislamu.

Wizara za Mashauri ya Kigeni za Kuwait na Qatar zimetoa taarifa kwa nyakati tofauti zikilaani hujuma na uvamizi huo.

Taarifa ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Kuwait imesema kuwa, hatua ya Wazayuni ya kuuvamia msikiti huo ni kuyavunjia heshi wazi na bayana maeneo matakatifu na niukiukaji wa wazi wa maazimio ya Umoja wa Mataifa, hati ya mkataba wa Geneva na mkataba wa haki za binadamu.

Kwa upande wake, Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Qatar sambamba na kulaani hujuma na uvamizi huo imesema kuwa, njama za Wazayuni zilizoratibiwa huko Quds zitapelekea kutokea mlipuko na kuanza tena machafuko. Qatar imeitaka jami ya kimataifa kuingilia kati matukio yanayojiri huko sasa huko Quds.

4088193

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha