Dkt. Ayyad, ambaye ni Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Mamlaka za Fatwa Duniani, alieleza kuwa kuvamiwa huko chini ya ulinzi mzito wa jeshi la Israel ni kitendo cha kiburi na muendelezo wa sera ya makusudi ya kuchafua na kudhalilisha maeneo matakatifu ya Uislamu.
“Matukio haya hayajatokea kwa bahati mbaya,” alisisitiza, “ni hatua zilizopangwa katika mpango mpana wa kuupokonya Msikiti wa Al-Aqsa asili yake ya Kiislamu na kuufanya sehemu ya urithi wa Uyahudi.”
Aliendelea kusema kuwa utawala wa Israel unalenga kutengeneza hali mpya kwa nguvu na unyanyasaji ili kufuta ukweli wa kihistoria na kuchochea hisia za mamilioni ya Waislamu duniani, ambao wameunganika kiroho na kihisia na msikiti huo.
Alionya kuwa ukiukaji wowote wa heshima ya Msikiti wa Al-Aqsa ni “kebehi dhahiri kwa imani na hisia za Ummah wa Kiislamu,” na akaongeza kwa msisitizo: “Tunasisitiza mara elfu: Msikiti wa Al-Aqsa na maeneo yote yanayouzunguka ni mali halali ya Uislamu. Hauwezi kugawiwa, kujadiliwa wala kupokonywa chini ya kisingizio chochote.”
Vilevile, Dkt. Ayyad alitoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa, mashirika ya kutetea haki za binadamu, na watu huru duniani kote kuchukua hatua thabiti na za haraka kupinga ukiukaji unaoendelea dhidi ya maeneo matakatifu na ardhi ya Palestina. Aliwahimiza kuunga mkono walioko mstari wa mbele katika mji wa al-Quds waliodhamiria kulinda heshima na urithi wa kiroho wa Ummah wa Kiislamu.
Uvamizi wa karibuni ulitokea Jumatatu asubuhi, walipovamia kwa kupitia lango la Wamagharibi, huku walowezi wakifanya matembezi ya kichokozi na ibada za Kitalmudi katika upande wa mashariki wa eneo hilo tukufu.
Wakati huo huo, majeshi ya Israeli yaliendelea kuweka vizuizi kwa Wapalestina wanaotaka kusali, kwa kukagua vitambulisho na kuzuia kuingia katika milango mbalimbali.
Msikiti wa Al-Aqsa, mojawapo ya maeneo matukufu zaidi katika Uislamu, umekuwa ukikumbwa na uvamizi wa karibu kila siku, isipokuwa Ijumaa na Jumamosi. Maafisa wa Palestina na viongozi wa Kiislamu wamekuwa wakitoa tahadhari kwa muda mrefu juu ya njama hizi zinazolenga kubadilisha hali halisi ya eneo hilo kwa mtindo wa kitawala wa kugawanya kimuda na kijiografia.
3493749