IQNA

Kikao cha Al Azhar kuhusu Al-Aqsa Katika Qur'ani

15:05 - April 13, 2025
Habari ID: 3480536
IQNA- Kikao cha kumi na nne cha kila wiki cha Tafsiri ya Qur'anI katika Msikiti wa Al-Azhar nchini Misri kitafanyika kwa mada "Msikiti wa Al-Aqsa katika Quran".

 

Rais wa zamani wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al-Azhar, Ibrahim al-Hudhud, na mkuu wa zamani wa Kitivo cha Lugha ya Kiarabu katika Chuo Kikuu cha Cairo watajadili mada hiyo.

Abdulmunim Fouad, msimamizi wa shughuli za kisayansi katika Msikiti wa Al-Azhar, amesema kuwa mkutano huu ni fursa muhimu ya kutafakari juu ya aya za Qur'ani na maana zake, na unafungua milango mipya ya utafiti kuhusu miujiza ya Qur'an.

 Aliongeza kuwa kikao hicho kitakuwa na athari katika kuimarisha uelewa wa kidini na kitamaduni wa washiriki kwa kuzingatia Msikiti wa Al-Aqsa na kinahimiza tafakari ya kina juu ya maandiko ya kidini.

Vikao hivi hufanyika kila Jumapili kila wiki, na kundi la wasomi na maprofesa wabobezi hutoa mihadhara.

Pia kuna muda wa maswali ya wazi na majadiliano kati ya washiriki, ambayo ni fursa ya mwingiliano na kubadilishana mawazo juu ya masuala mbalimbali.

4276114

Habari zinazohusiana
captcha