IQNA

Hujjatul Islam Muhsin Qara’ati

Tafsiri ya Qur’ani innatakiwa kueleweka kwa Umma

21:44 - August 27, 2022
Habari ID: 3475687
TEHRAN (IQNA) – Mwalimu na mfasiri mashuhuri wa Qur’ani Tukufu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anasema tafsiri za Qur’ani Tukufu zinapaswa kueleweka kwa umma na pia wakati huo huo kuwa na mvuto kwa wataalamu.

"Mtu hapaswi kudhani kuwa kadiri tafsiri inavyokuwa ngumu zaidi, ndivyo itakavyokuwa ya kitaalamu," Hujjatul Islam Muhsin Qara’ati aliiambia IQNA katika hafla iliyofanyika kuzindua vitabu vyake kadhaa katikati ya Julai.

Pamoja na hayo amesisitiza kuwa tafsiri zinapaswa kuwa na muundo ambao utawavutia wataalamu na watafiti.

Amebainisha kuwa maprofesa wawili wa sheria wa vyuo vikuu wamesema kwamba wamegundua pointi 2,600 kuhusu sheria katika Tafsir Noor ya Qur’ani Tukufu. Tafsir Noor ni tafsiri ya kina ya Qur’ani Tukufu iliyoandikwa na HujjatulIslam Qara'ati kwa lugha sahali.

 “Kuna baadhi ya vipengele ndani ya Quran ambavyo bado havijulikani. Hata herufi za maneno ndani ya Qur’ani huwa na maana ya kina; kwa mfano, unaposoma aya kuhusu wudhu utaona jinsi herufi inavyochukua nafasi katika kuelewa dhana yake,” aliongeza.

Mwanachuoni huyo pia alinukuu hadithi ya Imam Sadiq (AS) ambayo inabainisha kwamba kila ukurasa, neno, na herufi ya Quran hua na maana maalum. Hii inaonyesha umuhimu wa kusoma na kutafakari kuhusu  aya za Qur’ani, aliongeza Qara'ati.

"Kwa kusoma Qur’ani unahitaji mpango. Kwa mfano, mtu anaweza kutenga dakika chache kila usiku kusoma tafsiri ya Qur’ani ukiwa  na wanafamilia.

Pia aliwashauri Waislamu kujifunza neno moja au nukta moja ya Quran kila siku. "Usisahau kuwa Qur’ani ni tamu. Bado hatujaionja.

3480231

captcha