IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu Ufaransa

Ufaransa kuwatimua maimamu 15 wa misikiti

12:03 - September 01, 2022
Habari ID: 3475716
TEHRAN (IQNA)- Maimamu 15 wa msikiti huko nchini Ufaransa watafukuzwa nchini humo kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uchochezi.

Duru zinadokeza kuwa orodha ya maimamu watakaotimuliwa inatayarishwa katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ufaransa, na baadhi ya vyama vya kisiasa Ufaransa vinataka kushirikishwa katika kuitayarisha.

Orodha hii inajumuisha majina 15 ya maimamu wa misikiti ya nchi hiyo wanaotuhumiwa kwa kueneza chuki, ubaguzi na ukiukaji wa maadili ya jamhuri, na juhudi zinafanywa kuwafukuza nchini.

Vyanzo vilivyo karibu na Marine Le Pen, kiongozi wa chama cha misimamo mikali ya mrengo wa kulia, ambaye alishindwa na  Emmanuel Macron katika uchaguzi wa rais wa Ufaransa, amesema kwamba maimamu hao wa misikiti wanatoka nchi za Kaskazini mwa Afrika na nchi kama vile Morocco, Algeria na Tunisia.

Siku chache zilizopita, kufuatia ombi la Waziri wa Mambo ya Ndani, mfumo wa mahakama wa Ufaransa ulikuwa umetoa mwanga wa kijani kumfukuza mmoja wa maimamu waliokuwa karibu na harakati ya Misri ya Ikhwanul Muslimin.

captcha