IQNA

Maadili mema ya Kiislamu

Dereva wa Teksi Muislamu Uingereza apongezwa kwa kuokoa maisha ya abiria

13:48 - September 08, 2022
Habari ID: 3475750
TEHRAN (IQNA) – Dereva wa teksi Muislamu huko Derby, Uingereza, amepongezwa kwa kuokoa maisha ya abiria wake mmoja.

Akiongoza kwa mfano, dereva wa teksi Muislamu aliokoa maisha ya abiria, na kumpeleka hospitalini baada ya kuanguka alipokuwa akshuka kwenye teksi yake.

Abdul Majid alikuwa akiwaendesha wanaume wawili kuelekea Barabara ya Duffield mwendo wa saa 10:30 jioni Jumamosi, Agosti 13. Baada ya kutoka nje ya gari, mtu huyo alipiga hatua chache na ghafla alianguka katikati ya barabara, akaanguka na kupoteza fahamu na kuumia bega.

"Mhudumu wa dharura alisema mtu huyo alihitaji kwenda hospitalini lakini hakukuwa na ambulensi. Kwa hivyo nikasema, naweza kumchukua, kwa hivyo nikampeleka kwenye A&E na mshirika wake,” Abdul Majid amewaambia waandishi habari.

"Lakini niliwaambia, ilikuwa jukumu langu kama mwanadamu, kwa hivyo sikutaka malipo, lakini walisema lazima wanipe, kwa hivyo walituma kadi yenye Pauni 100.

"Tunapaswa kusaidiana katika hali hii. Binadamu tunapaswa kusaidiana.”

Ateeq Naseem, meneja katika Albatross Teksi, alisifu mawazo ya haraka ya Majid na kusema "sio mashujaa wote hutambuliwa waziwazi".

"Wanandoa hao walitoa shukrani sana hivi kwamba Abdul alitumia saa nyingi pamoja nao. Abdul alichukua hatua. Yeye ni shujaa mnyenyekevu sana."

Mnamo Septemba 2021, mwanamume Mwislamu huko North Leigh, Oxfordshire, alisifiwa kwa kufaulu kuokoa majirani zake wakati moto ulipoanza katika nyumba yao.

Azz Mahmoud, mfanyakazi wa vijana wa Kiislamu mwenye umri wa miaka 37 huko Oldham, alifanya CPR kwa mara ya kwanza kabisa kuokoa maisha ya mtu.

3480395

captcha