IQNA

Waislamu Uingereza

Ripoti : Waislamu Uingereza wameshushwa hadhi na kuwa raia wa 'Daraja la Pili'

15:20 - September 12, 2022
Habari ID: 3475771
TEHRAN (IQNA) – Kwa mujibu wa ripoti ya taasisi moja ya utafiti, Waislamu wa Uingereza wamepunguziwa hadhi ya uraia wao hadi hadhi ya "daraja la pili" kutokana na mamlaka iliyoongezwa hivi karibuni ya kuwavua watu utaifa au uraia wao.

Taasisi ya Mahusiano ya Rangi Uingereza (IRR) inasema walengwa wa mamlaka kama hayo ni takriban Waislamu pekee, wengi wao wakiwa ni wa turathi za kusini mwa Asia, kupachika ubaguzi na kuunda aina ndogo ya uraia.

Ripoti ya IRR ilichapishwa siku ya Jumapili huku kukiwa na utata mpya kuhusu kesi ya Shamima Begum, ambaye alisafirishwa kinyemela mikononi mwa Daesh akiwa na umri wa miaka 15, na kwa kuzingatia Sheria ya Utaifa na Mipaka - iliyoruhusu uraia kuvuliwa kisheria bila kumjulisha mhusika.

Frances Webber, makamu mwenyekiti na mwandishi wa ripoti wa IRR, aliandika: "Ujumbe uliotumwa na sheria juu ya kunyimwa uraia tangu 2002 na utekelezaji wake kwa kiasi kikubwa dhidi ya Waislamu wa Uingereza wa turathi za Asia ya Kusini ni kwamba, licha ya hati zao za kusafiria, watu hawa hawana na wanaweza kuonekana kama raia 'wa kweli', kama walio na asili ya Uingereza walivyo.

"Wakati raia mzungu mwenye asili  ya Uingereza, ambaye hana uraia mwingine, anaweza kufanya uhalifu mbaya zaidi bila kuhatarisha haki yake ya kubaki Mwingereza, Waislamu raia wa Uingereza wanaokadiriwa kuwa milioni 6 ambaye asili yao ni nchi nyingine hawana uhakika kuwa uraia wao ni wa kudumu."

Webber alisema kabla ya kutumiwa dhidi ya mhubiri Muislamu Abu Hamza mwaka 2003, sheria ya kupokonya uraia  haikuwa imewahi kutumiwa kwa miaka 30. Lakini tangu wakati huo kumekuwa na kesi angalau 217, ambapo  104 walipokonywa uraia mwaka 2017 baada ya kuanguka kwa kundi la kigaidi la Daesh nchini Syria.

Licha ya madai ya serikali kwamba mamlaka yanatumiwa tu dhidi ya wale ambao ni tishio kubwa kwa usalama wa taifa, au ambao wamefanya uhalifu wa kuchukiza, ripoti zinasema Waislamu wanatazamwa kama raia wa  "daraja la pili, na uraia wao unaweza kubatilishwa wakati wowote.

Ikinukuu mpango wa 'kukabiliana na ugaidi', ambao umegubikwa na madai ya kuwa ni siri ya kupeleleza jumuiya za Kiislamu, ripoti hiyo ilisema kuwanyima uraia ni "kipengele kimoja tu cha hatua zinazolenga jumuiya za Kiislamu, na sasa hali hiyo imepelekea Waislamu wa Uingereza kuwa 'jamii inayoshukiwa'”.

3480449

Kishikizo: waislamu ، uingereza ، raia ، daraja la pili
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha