IQNA

Uislamu barani Ulaya

Mwanamke wa Uingereza asilimu baada ya kusoma Qur’ani mara Nne

21:52 - September 03, 2022
Habari ID: 3475726
TEHRAN (IQNA) – Mwanamke mmoja huko Plymouth, kusini magharibi mwa Uingereza, alikubali Uislamu baada ya kusoma Qur’ani Tukufu mara nne katika muda wa mwezi mmoja.

Aliinukia akiwa Mkristo. Uamuzi wake uliwafanya marafiki na familia yake kushangazwa na hata nyanyake aliita mabadiliko yake ya imani kuwa ya muda mfupi.

Wakati jumuiya ya Kiislamu ni ndogo huko Plymouth, wakati wa  Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wanawake watatu walikubali Uislamu.

Maryam alikulia katika familia ya Kanisa la Kikristo la Uingereza na hivyo alikuwa akiwamini Mungu sikuzote. Wakati wa ujana wake alianza kuyumba-yumba, hakuweza kuelewa kwa nini ankwenda kanisani kila Jumapili.

Hatimaye, baada ya utafiti, Maryam  alitamka Shahada Mbili katika Kituo cha Kiislamu cha Uchamungu, na hivyo akatangaza rasmi kuwa Muislamu miezi michache iliyopita.

Shahada ni tamko la imani, ambalo hutamkwa na Yule ambaye anataka kusilimu au kuingia katika imani ya Kiislamu. Maneno ya wakati wa Shahada yanatafsiriwa kuwa, “Nashuhudia kwamba hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu, na ninashuhudia kwamba Muhammad ni mjumbe wa Mungu.”

Alisema aliukaribia Uislamu hatua kwa hatua, baada ya kusoma kufanya utafiti kuhusu Uislamu, Ukristo na Uyahudi. Hatahivyo anasema uamuzi wake wa kufanya utafiti zaidi kuhusu Uislamu ulikuja wakati wa mazungumzo na fundi umeme ambaye alikuja kurekebisha kitu ndani ya nyumba yake baada tu ya shambulio la bomu la Manchester. Alisema: "Nilikuwa nikipitia simu yangu na nikasema 'hii ni mbaya sana' na namkumbuka akijibu, 'hiyo ni wazi kabisa, unaonaje kuhusu Waislamu wa kawaida?' na nikasema simfahamu Muislamu yeyote. ”  Maryam anasema mazungumzo hayo yalimfanya achunguze zaidi Uislamu.

Wakati wa Ramadhani mwaka huu, Maryam alisoma tafsiri ya Kiingereza ya  Qur’ani Tukufu- kitabu kitakatifu cha Kiislamu - mara nne  huku akifanya utafiti zaidi katika sehemu ambazo hakuelewa. Alisema: “Mwanzoni nilitaka kufanya utafiti kuhusu aya za Qur’an kwani  unapata watu ambao wamechota vipande vya Qur’ani na kusema Uis lamu ni dini yvurugu na chuki.

"Kwa hivyo nilitaka kuona ilichosema na kwa kweli, sikupokea ujumbe wa vurugu katika aya za Qur’ani. Niliendelea kufikiria lazima kuwe na kitu ndani yake kwani ndiyo dini inayokua kwa kasi zaidi ulimwenguni.”

"Bibi (nyanya) yangu anadhani kusilimu kwani ni 'awamu,' tu na hivyo hatuzungumzii suala hili kwani linamkasirisha. Si hali nzuri kwa mama yangu lakini anafurahi kuwa nimepata sehemu ambayo nahisi naistahiki maishani.”

"Kwa kweli, nimehisi upinzani zaidi kutoka kwa marafiki au wale walio kanisani ambao wameamua kufikiria kuwa kuna  "mtu amenifanyia hivi, mtu amenibadilisha.”

"Nadhani ni vigumu kwa watu wengi kuamini kuwa hili ni chaguo langu, kulikubali. Imani yangu inanifanya nijisikie mwenye furaha na kutosheka, naendelea kufikiria Mwenyezi Mungu ni mkubwa kuliko matatizo yetu yote bila kujali kitakachotokea."

Aidha anasema: “Ninapokuwa  msikitini naona wanawake wote ni wa kirafiki na wakaribishaji wa kweli, wamefahamiana kwa muda mrefu kuliko walivyonifahamu lakini sijawahi kuhisi kama mtu wa nje."

3480323

captcha