IQNA

Janga la COVID-19

Waumini katika Misikiti ya UAE ruhsa kusali bila barakoa, vizuizi vya COVID-19 vyaondolewa

14:31 - November 09, 2022
Habari ID: 3476061
TEHRAN (IQNA) - Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi 28, Waislamu katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) wanaweza kusali bila barakoa huku wakuu wa afya wakitangaza kuondolewa kwa takriban vizingiti vyote vya COVID-19.

UAE ilikuwa ilianza kuchukua hatua kali kuzuia maambukiz ya COVID-19 mnamo Machi 16, 2020. Ili kuwaweka wakaazi wake salama kutokana na janga hili, misikiti kote nchini ilifungwa kwa waumini kwa muda wa miezi kadhaa. Sasa hali imebadilika baada ya zaidi ya miaka miwili.

"Leo, tulitangaza kuondoa vizuizi vyote vya COVID-19 na kuvaa barakoa katika vituo vyote vilivyo wazi na vilivyofungwa, pamoja na mahali pa ibada na misikiti," Saif Al Dhaheri wa Mamlaka ya Kitaifa ya Dharura na Usimamizi wa Maafa.

Imamu wa Msikiti wa Jumeirah alisema, "Ni hatua ya nzuri sana; msikiti sasa uko wazi kama ilivyokuwa siku za kabla ya janga."

Kuswali kwenye mikeka ya kibinafsi itakuwa ni hiari kwenye misikiti na vituo vya kusalia. Imran, muumini mmoja msikitini alisema, "Kusali kwa uhuru msikitini bila ya kuzingatia miongozo ya tahadhari ni nafuu."

Wasimamizi wa Misikiti na Maimamu walifanya kazi ya kupongezwa kuhakikisha kwamba itifaki za COVID-19 zinafuatwa na kuzingatiwa na waabudu wote. Abdul, mlinzi wa msikiti, alisema, "Kwetu sisi, usalama wa mahali patakatifu ulikuwa kipaumbele cha kwanza; tulipaswa kuhakikisha kila mtu anaingia na mikeka yake ya kibinafsi na barakoa."

3481177

Kishikizo: uae barakoa covid 19
captcha