IQNA

Sala katika Msikiti Mkuu wa Makkah bila kuzingatia kanuni ya corona ya kutokaribiana

16:32 - March 07, 2022
Habari ID: 3475017
TEHRAN (IQNA) – Waumini katika Msikiti Mkuu wa Makkah Jumapili walisali Sala ya Alfajiri bila kuzingatia kanuni ya corona ya kutokaribiana ikiwa ni mara ya kwanza kufanya hivyo baada ya muda mrefu.

Hatua hiyo imekuja baada ya uamuzi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudi kuondoa kanuni zilizokuwa zinatakelezwa za kuzuia kuenea corona zikiwemo za kutokaribiana waumini  Msikiti Mkuu wa Makkah, Msikiti wa Mtume SAW mjini Madina na misikiti mingine. Aidha si sharti tena waumini kuvaa barakoa.

Msikiti Mkuu unatoa mazingira ya kiafya na salama, ambapo Ofisi ya Rais wa Masuala ya Misikiti Miwili Takatifu husafisha viyoyozi ndani ya Msikiti Mkuu mara tisa kwa siku na pia hewa husafishwa kwa mionzi ya ultraviolet kabla ya kuisambaza msikitini kupitia vifaa maalum ambayo kusafisha hewa asilimia 100% kupitia hatua kadhaa.

Hatua hizo ni pamoja na kutoa hewa ya asili kutoka kwenye paa la Msikiti Mkuu kupitia feni za kufyonza, ambapo hewa inasukumwa kwenye vichungi vinavyosafishwa kila siku kabla ya hewa kufika kwenye vitengo vya kupozea.

Pia, zaidi ya wafanyakazi 4,000 wanaendelea kuusafisha Msikiti Mkuu mara 10 kwa siku kwa kutumia mashine za kisasa zaidi  ili kuhakikisha afya na usalama wa waabudu wanapofanya ibada na sala.

3478071

Kishikizo: makkah msikiti Corona
captcha