IQNA

Wapalestina wa Gaza

Wapalestina wa Gaza waliohifadhi Qur’ani wakiwa katika jela ya Israel waenziwa

22:28 - December 01, 2022
Habari ID: 3476180
TEHRAN (IQNA) – Katika sherehe huko Gaza, wafungwa 77 wa Kipalestina ambao wameweza kuhifadhi Qur’ani Tukufu wameenziwa.

Hafla hiyo iliandaliwa na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, na kituo cha kusaidia wafungwa wa Kipalestina huko Gaza.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na familia za waliohifadhi Qur’ani  pamoja na maafisa wa Palestina na shakhsia wa harakati za mapambano ya Kiislamu au muqawama.

Ali al-Amudi, mkuu wa idara ya mawasiliano ya Hamas huko Ghaza, alisoma taarifa ya kusifu kazi kubwa ya wafungwa hao ya kuihifadhi Qur'ani Tukufu huku wakizuiliwa katika magereza ya kuogofya ya utawala dhalimu wa Israel.

Ismail Haniyeh, mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas, alizungumza  katika hafla hiyo ambaye aliwapongeza wafungwa kwa kuwa na silaha za imani.

Pia alisisitiza ahadi ya Hamas ya kuwasaidia wafungwa kurejea makwao. Kwa mujibu wa takwimu za Wapalestina, kuna karibu wafungwa 4,550 wa Kipalestina katika jela za utawala haramu wa Israel, wakiwemo watoto 175 na wanawake 27.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotangazwa ni kuwa, takribani Wapalestina milioni 1 wametipia tajiriba ya kushikiliwa mateka katika magereza ya Israel kuanzia mwaka 1967 hadi sasa. Idadi hii inaundwa asilimia 20 ya taifa la Palestina. Kwa msingi huo, suala la mateka wa Kipalestina ni hasasi na nyeti mno la linaweza kusababisha kutokea mlipuko wa hali ya mambo katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Gaza.

4103813

Kishikizo: gaza ، wapalestina ، kuhifadhi qurani
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha