IQNA

Kuhifadhi Qur'ani Tukufu

Mvulana Mpalestina wa miaka 7 ahifadhi Qur'ani kikamilifu Gaza

15:40 - May 24, 2022
Habari ID: 3475288
TEHRAN (IQNA)- Rashad Nimr Abu Ras, mvulana Mpalestina mwenye umri wa miaka saba amehifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu katika Ukanda wa Gaza.

Mvulana huyo ambaye amemaliza darasa la kwanza katika shule moja ya msingi Gaza amepata umashuhuri kwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.

Katika picha zilizo hapa chini, Rashad, akiwa ameandamana na familia yake, alitahiniwa na  maulamaa wa Qur'ani Tukufu ambao walithibitisha kuwa amehifadhi Qur'ani Tukufu kihamilifu.

Nimr, baba yake Rashad amesema alimhimiza mwanae kwa kumpa zawadi kila aliopohifadhi kurasa kadhaa za Qur'ani.  Alianza kupata zawadi kadhaa kama mpira na hatimaye akapata zawadi ya baiskeli kutokana na jitihada zake za kusoma na kuhifadhi Qur'ani.

Hatua kwa hatua Rashad alikuwa  anahifadhi Qur'ani hata bila ya kupewa zawadi na aliendelea kupata motisha kutoka kwa wazazi, walimu na majirani.

Katika hafla iliyohudhuriwa na idadi kubwa ya wasomi na wanasiasa wa Gaza, Rashad alitambuliwa rasmi kama Hafidh Qur'ani Tukufu na akapokea zawadi kadhaa ikiwa ni pamoja na Msahafu.

 
3479039
Habari zinazohusiana
Kishikizo: gaza qurani tukufu
captcha