IQNA

Ukanda wa Gaza

Kikao cha kuhitimisha Qur'ani Tukufu chafanyika Gaza

15:11 - August 24, 2022
Habari ID: 3475672
TEHRAN (IQNA) – Mkusanyiko wa waliohifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu ulifanyika katika Ukanda wa Gaza ambapo washiriki walihitimisha Qur'ani.

Kikao hicho ambacho kinajulikana kama 'Waliobora katika Kuhifadhi Qur'ani' kiliandaliwa na Kituo cha Gaza Dar-ol-Quran na Sunnah.

Zaidi ya wanaume na wanawake 500 ambao wamehifadhi Qur'ani walishiriki katika hafla hiyo huko Gaza siku ya Jumanne.

Msikiti wa Taqawi uliopo katika Kitongoji cha Sheikh Ridhwan a uliendesha programu hiyo kwa wanaume huku programu ya wanawake ilifanyika katika Msikiti wa Shafei katika Kitongoji cha Zaytoon.

Usomaji wa Qur'ani ulianza baada ya Sala ya Alfajiri na ukahitimishwa baada ya Swalah ya Alasiri.

Bilal Imad, Mkuu wa kituo hicho, alisema siku hii imetengwa kuwa siku ya kusoma Qur'ani Tukufu kikamilifu  kuanzia asubuhi hadi jioni kila mwaka.

Alitumai kuwa kutakuwa na idadi kubwa zaidi ya watu watakaoshiriki katika mpango huo mwaka ujao.

Imad ameongeza kuwa kituo hicho kimepokea barua za shukurani  kutoka nchi mbalimbali kwa kuendesha programu hiyo ya Qur'ani.

Shughuli za Qur'ani ni za kawaida sana katika Ukanda wa Gaza na programu za usomaji na kuhifadhi Qur'ani hufanyika katika eneo hilo mwaka mzima. Pamoja na kuwa kwa zaidi ya miaka 15 sasa  Ukanda wa Gaza uko chini ya mzingiro wa kinyama wa utawala wa Kizayuni lakini Wapalestina katika eneo hilo wanafungamana kikamilifu na harakati za Qur'ani Tukufu.

 

 

4080249

Habari zinazohusiana
captcha