IQNA

Waislamu Uingereza

Ufafanuzi Mpya wa 'Msimamo Mkali' nchini Uingereza walenga Waislamu

15:13 - March 24, 2024
Habari ID: 3478568
IQNA - Ufafanuzi wa hivi majuzi wa itikadi kali uliopendekezwa na serikali ya Uingereza umelaaniwa kwa kuwalenga Waislamu nchini humo.

Zaidi ya maimamu 400 na wanazuoni wa kidini wameshutumu ufafanuzi huo.

Katibu wa jumuiya za mrengo wa kulia Michael Gove wiki iliyopita alifichua tafsiri yenye utata ya "itikadi kali" ambayo inalenga zaidi ya Waislamu milioni 3.5 wa Uingereza na imani ya Kiislamu.

Gove aliangazia mahususi mashirika kadhaa ya Kiislamu, kama vile Jumuiya ya Waislamu wa Uingereza (MAB) na Cage, akisema kuwa serikali inakusudia kuyachunguza chini ya ufafanuzi huo mpya kutokana na "mwelekeo wao wa Uislamu."

Katika barua ya pamoja, maimamu waliandika kwamba Gove ana historia ya kulenga Uislamu na Waislamu na anajulikana kwa kampeni dhidi ya Waislamu kwa kushirikiana na wabaguzi wa rangi na wenye chuki dhidi ya Uislamu au Islamophobes.

"Tunatambua kuwa mjadala wa 'itikadi kali' unategemea dhana mbovu na isiyo na msingi kielimu ya kihafidhina kwamba itikadi ni sababu ya vurugu za kisiasa," wameandika katika barua hiyo.

Aidha wamesema: "Inaonekana msukumo wa msingi wa tangazo hili ni kutoridhika miongoni mwa wahafidhina mamboleo, wanaoiunga mkono Israel ndani ya serikali kufuatia wimbi la harakati halali zinazopinga uvamizi wa Israel na Wazayuni dhidi ya Palestina, hususan, Gaza."

Baraza la Waislamu la Uingereza (MCB), ambalo ndilo shirika kubwa zaidi linalowakilisha Waislamu nchini Uingereza, lilielezea wasiwasi wake wiki iliyopita kuhusu uwezekano wa kulengwa kwa baadhi ya mashirika tanzu chini ya ufafanuzi uliopendekezwa.

3487701

Habari zinazohusiana
captcha