IQNA

Historia

Je! Safina ya Nuhu iko Mashariki mwa Uturuki?

18:42 - December 08, 2022
Habari ID: 3476215
TEHRAN (IQNA) – Watafiti wanafanya kazi ya uchimbaji katika eneo nchini Uturuki ambapo mabaki ya safina ya Nuhu yanaaminika kuwepo.

Hadithi ya chombo hiki cha usafiri majini imeelezwa katika Torati, Biblia na Qur’ani Tukufu.

Timu ya utafiti iliyoanzishwa na Chuo Kikuu cha Ağrı Ibrahim Çeçen (AIÇU) na Chuo Kikuu cha Ufundi cha Istanbul (ITU) ilianza kufanya kazi kwa pamoja katika wilaya ya Ağrı mashariki mwa Uturuki. Sampuli zinazochunguzwa ni pamoja na vipande vya udongo na miamba na zilipatikana katika eneo hilo na watafiti, ambao ni pamoja na wanataaluma ambao ni wataalam wa jiofizikia, kemia na geo-akiolojia. Sampuli zimetumwa katika maabara za ITU kwa uchunguzi.

Mabaki katika eneo hili yaligunduliwa kwa mara ya kwanza na mhandisi wa ramani Kapteni Ilhan Durupınar mwaka wa 1959 wakati wa safari ya ndege ya upelelezi ili kupata ramani ya eneo la mashariki la Anatolia. Mabaki hayo sasa yanavutia watalii wengi wa ndani na nje ya nchi.

Katika Qur’ani Tukufu, imetajwa kuwa Mwenyezi Mungu alimjulisha Nabii Nuhu kuhusu gharika inayokuja ambayo ingeifunika dunia nzima ili kumuokoa yeye na wale wote walio pamoja naye katika safina yake. Kisha Nuhu akajenga chombo chake ambamo aliweka watu watiifu wa familia yake pamoja na jozi za wanyama na ndege wote.

Eneo hilo liko hatarini kwani linatishiwa na maporomoko ya ardhi na kwa msingi huo,  "Timu ya Utafiti wa Mlima wa Ağrı na Safina ya Nuhu" iliundwa kwa ushirikiano kati ya AIÇU na ITU kwa ajili ya utafiti wa kisayansi kufanywa juu ya magofu.

Makamu Mkuu wa AIÇU Faruk Kaya alibainisha kuwa walianzisha utafiti juu ya Safina ya Nuhu na kusema: "Mlima Ararat ni mlima unaojulikana duniani kutokana na sifa zake za kijiolojia na kijiomofolojia, na pia kulingana na imani kwamba ni nyumbani kwa Safina ya Nuhu. . Chuo kikuu chetu kimekuwa kikifanya kazi katika eneo hili tangu 2003. Mwaka huu, tulitaka kufanya kazi na ITU kufanya masomo ya kina zaidi."

"ITU ni mojawapo ya vyuo vikuu vilivyo na vifaa vingi katika suala hili. Tuliunda kikundi kazi cha wasomi kutoka chuo kikuu na walichunguza muundo wa asili kati ya vijiji vya Telçeker na Üzengili, yaani, muundo unaofanana na muundo wa Safina ya Nuhu. Sampuli zinachunguzwa, tutaamua mchakato kulingana na matokeo.Tuna wakufunzi wataalam walio na vifaa maalum na uwezo wa jiofizikia, kemia na utafiti wa kiakiolojia," aliongeza.

Akibaini pia kwamba Safina ya Nuhu inawavutia wengi ulimwenguni, Kaya alisema: "Safina ya Nuhu inatajwa katika vitabu vitakatifu vya dini za Mwenyezi Mungu. Vyanzo vingi vinavuta fikira kwenye Mlima Ararati na mazingira yake, eneo hilo lina uwezekano mkubwa sana wa utalii wa kiimani. Hasa, kuna shauku inayoongezeka kutoka nchi za Ulaya na Amerika. Wazungu tayari wameanzisha masomo ya kwanza katika uwanja huu kwani Johann Jacob Friedrich Wilhelm Parrot alipanda Mlima Ararati kutafuta mabaki ya Safina ya Nuhu mnamo 1829."

"Mwaka 2008, kikundi cha watafiti kutoka Hong Kong walikwenda kwenye Mlima Ararat. Walikuta pango humu ndani na baadhi ya mbao ambazo walidai kuwa ni za Safina ya Nuhu. Bila shaka, ikiwa mbao walizozipata ni za Safina ya Nuhu ni suala lenye utata, lakini tunadhani walifanikiwa kwa upande mwingine. Huko Hong Kong walijenga jumba la makumbusho la Safina ya Nuhu, ambalo limetembelewa na mamilioni ya wageni. Kiuchumi waliweka walitekeleza kivitendo utalii wa kiimani. Ağrı , ambayo ni moja ya mikoa yenye maendeleo duni ya nchi yetu, ina uwezo mkubwa kwa maana hiyo. Lengo letu, kama chuo kikuu, ni kwamba ikiwa tunaweza kugeuza eneo hili kuwa kituo cha utalii wa imani," aliongeza.

Kishikizo: uturuki ، safina ya nuhu
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha