IQNA

Mazungumzo baina ya dini

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa asema amavutiwa kiroho katika Haram ya Imam Hussein AS

21:45 - December 23, 2022
Habari ID: 3476293
TEHRAN (IQNA) - Mjumbe wa Umoja wa Mataifa amesema amepata mvuto wa kipekee wa kiroho alipokuwa akitembelea Haram (kaburi) takatifu ya Imam Hussein (AS) huko Karbala, Iraq.

Jeanine Antoinette Plasschaert, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, alitembelea eneo hilo takatifu  mnamo Desemba 11, 2022.

Baadaye katika barua kwa Mfawidhi wa Haram Takatifu ya  Imam Hussein AS, aliwashukuru wasimamizi wa eneo hilo kwa upokezi bora na kwa ukarimu wao. "Huu ulikuwa uzoefu mzuri wa kiroho," alisema katika barua iliyoandikwa kwa Kiarabu.

Pia alipongeza shughuli za kibinadamu za Warith International Foundation for Oncology huko Karbala ambayo ina uhusiano na Mfawidhi wa Haram Takatifu ya  Imam Hussein AS.

UN Envoy Lauds Her Great Spiritual Experience at Imam Hussein Shrine

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa pia ulifanya mkutano na Ayatullah Sistani siku chache kabla ya kutembelea eneo hilo takatifu.

Katika mkutano huo, mwanazuoni wa Kiislamu alisisitiza umuhimu wa juhudi zilizoratibiwa kukuza utamaduni wa kuishi pamoja kwa amani, kukataa vurugu na chuki, na kudumisha maadili ya mshikamano unaozingatia haki na kuheshimiana kati ya wafuasi wa imani tofauti.

Ayatullah Sistani aidha amesema majanga ambayo mataifa mengi na makundi ya kikaumuna kijamii yanakumbana nayo katika maeneo mengi ya dunia yanatokana na dhulma na ukosefu wa uadilifu wa kijamii ambapo yana nafasi kubwa katika kuibuka baadhi ya makundi yenye misimamo mikali yanayotekeleza dhidi ya raia wasio na ulinzi.

4108943

captcha